
Msichana wa Maisha Yangu
Kuna fumbo kubwa ambalo limeachwa na kijana Steven wakati anatoka kijijini Usuka, Njombe kuelekea Dar kutafuta maisha. Tatizo la ajira lilikuwa ni wimbo wa taifa jambo aliloamua kulivalia njuga kulitatua kupitia kipaji alichopewa na Mungu. Matokeo yake alikutana na utofauti hasa kwenye kila idara, alichanganyikwa na kukosa chaguo kipi afanye. Hii ni simulizi ambayo itakupa majibu kuhusu kutimiza ahadi, teknolojia na malipo ya juhudi isiyokuwa ya kawaida.