
Zawadi ya upendo inabebwa na mengi ipo hivyo na katika yote hayo kuna maumivu. Unaambiwa poteza mengi lakini usipoteze matumaini kwa kuwa kila hatua ina hesabika kuwa na matokeo chanya. Upendo wake kwa binti Monica haukufichika na aliamini angerejea na kuishi naye katika ulimwengu wa furaha. Ni kweli Kelvin aliondoka Njombe na kwenda mjini Dar, alipopata muda kurejea alichokutana nacho kilileta visa na simulizi hii ambayo ukianza kufungua ukurasa wa kwanza utapenda kuendelea nayo mpaka ukurasa wa mwisho, usiikose...