
ACHA KUJISUBIRISHA
Je, ni kweli unashindwa kufanikiwa, au umezoea kujizuia mwenyewe?
Umewahi kuwa na wazo zuri lakini ukashindwa kulifanyia kazi? Umewahi kupanga kuanza biashara, kujifunza ujuzi mpya au kubadilisha maisha yako, lakini ukaishia kusema “Nitaanza kesho”?
Ukweli ni kwamba, wakati mwingine kikwazo kikubwa kinachokuzuia kusonga mbele si ukosefu wa pesa, elimu au fursa, bali ni maneno unayojirudia kila siku.
Kitabu hiki kitakusaidia kutambua kauli 4 zinazoweza kukufanya uendelee kuahirisha ndoto zako, kupoteza fursa na kubaki pale pale.
Ndani ya kitabu hiki utajifunza:
- Kutambua kauli zinazokuzuia kuchukua hatua.
- Kuacha tabia ya kuahirisha mambo muhimu.
- Kujenga ujasiri wa kuanza hata kama hujakamilika.
- Kubadilisha fikra zako na kuanza kuchukua hatua kuelekea malengo yako.
Ujumbe muhimu wa kukumbuka
"MAISHA YAKO HAYAWEZI KUBADILIKA IKIWA KILA SIKU UNAENDELEA KUTOA SABABU ZA KUTOKUANZA."
Usisubiri mazingira yakamilike. Usisubiri uwe na kila kitu. Anza na kile ulicho nacho, ulipo, na hatua ndogo unayoweza kuchukua leo.
SOMA. BADILIKA. CHUKUA HATUA.