
Ahadi inapowekwa lengo ni kuitimiza kwa namna yoyote ile, hicho ndicho kilikuwa kwenye kichwa cha Christopher baada ya kuipokea kwa mikono miwili ahadi kutoka kwa msichana Irene. Ilikuwa ahadi ngumu ila alijipa moyo akiamini kwamba ikifika kesho, yote yatatimia na furaha yao itaendelea kudumu daima katika safari ya maisha yao, hivyo tu basi.
Ule uwezo wao kila mmoja alionyesha hali ya kujali na upendo ulionekana dhahiri. Kila upande ulikuwa unaonyesha unaonyesha picha moja ambayo inaeleweka na kutazamika kwa tabasamu ila ilikuja siku ambayo hakuna aliyetarajia ilipotokea.
Ni mume, Irene alipewa chaguo la wazazi wake wakimtaka kuolewa na mwanaume mwingine, George. Siku Irene anavalishwa pete ya uchumba na George, Christopher anahudhuria tukio hilo na kutoa maneno mazito sana kwa Irene