
Tangu mwanzo, Mungu aliwapa wanadamu uwezo wa kuchagua. Hatukuumbwa kama mashine zisizo na hiari (roboti). Ndiyo maana, hata alipotoa amri zake, bado binadamu walikuwa na nafasi ya kutii au kutokutii. Kwa bahati mbaya, uamuzi wa kwanza wa mwanadamu kufanya ulikuwa wa kutotii
Kitabu hiki kimeandikwa kuwasaidia vijana na wahitimu wa vyuo kuelewa kwamba maamuzi si vitendo tu—ni mbegu zinazopandwa katika udongo wa kesho. Katika dunia ya leo, vijana hukabiliwa na shinikizo nyingi: marafiki, mazingira, hisia na ukosefu wa maarifa ya kutosha. Mara nyingi nguvu hizi huwasukuma kufanya maamuzi ya haraka au ya kizembe, ambayo baadaye hubeba mzigo mzito wa majuto.