
Mungu alipotuumba wanadamu alituwekea na vipimo vya kutupima ili kutujua kama kweli tunaweza kufuata au kuishi kwa kufuata maelekezo yake. Hata mzazi anapotaka kumpa kitu mwanaye, jambo la kwanza atampa mtihani mwanaye kumpima kujua jambo fulani na atakapojiridhisha basi atampatia kitu hicho. Ndani ya hadithi kii kuna kisa cha mtu aitwaye Martin ambaye alikutana na visa na mikasa mingi katika maisha yake. Mungu alimpima kwa namna aliyoona inafaa na baada ya vipimo hivyo ushindi wa kishindo ulipatikana wakati ambao anataka kukata tamaa. Nakusihi ufuatilie kisa cha mtu huyu, utajifunza, utaelimika, utaonyeka na utamaliza kusoma hadithi hii ukiwa na mtazamo mpya na elimu mpya juu ya masuala kadha wa kadha katika maisha.