
Ni ukweli usiopingika kuwa moja ya tamaduni ambayo tumerithi katika kutengeneza utambulisho wa mtu ama kitu ni majina ambayo tunaamini sana yakiwa yemetoka kwenye kitabu kitakatifu Biblia. Jina ni utambulisho, hivyo kwa kutumia jina lililoko ndani ya biblia ni sawa na kujitambulisha kuwa wewe ama kitu chako ni wa mlengo wa kikristo
Kitabu hiki kinaangazia maana zilizoko nyuma ya majina yaliyotumika ndani ya biblia kwa kuangalia asili yake, yapo majina yenye maana nzuri lakini yapo pia yenye maana mbaya, yapo ya kumtukuza Mungu na mengine ya kutukuza miungu, mfano jina ABEDNEGO maana yake ni “mtumishi wa Nego” na huyo Nego alikuwa ni mungu wa hekima wa kibabiloni, ambae mfalme Nebukadneza alikuwa anamuabudu, hivyo ukisema tu jina liko kwenye biblia unalichukua bila kufatilia maana na chimbuko lake unaweza kuabudu miungu na kumkosea Mungu kupitia jina lako ama jina “DIANA” lina asili ya kilatini na maana yake ni Mwanga kamili jina la mungu wa kike wa kirumi aliejihusisha zaidi na mwezi pamoja na uwindaji.
Kupitia kitabu hiki, utajifunza maana za majina haya na jinsi yanavyohusiana na imani za Kikristo. Kwa kufahamu maana za majina haya, tunaweza kuelewa zaidi urithi wetu wa imani na jinsi historia ya Biblia inavyoathiri maisha yetu leo. Kitabu hiki ni mwongozo mzuri kwa wale wanaotaka kuchunguza zaidi asili ya majina yao na jinsi yanavyohusiana na imani zao.