Kitabu Nakala Ngumu : Tambua nguvu ya asili
Physical

Kitabu Nakala Ngumu : Tambua nguvu ya asili

1
TSh15,000.00

Je, Unajua Kuwa Kuna Vitu Kwenye Maisha Yako Vinasukumwa na Siri ya Asili Yako?


Kama Mkristo, huenda umekuwa ukipitia mapambano, vikwazo, au hata baraka fulani bila kuelewa chimbuko lake. Kuzaliwa kwenye familia yako, ukoo wako, au kabila lako sio bahati mbaya. Mungu Mwenyewe ndiye aliyekuchagulia asili hiyo. Lakini, je, unajua kuwa kuna nguvu, baraka, na mifumo ya asili iliyobebwa kwenye damu yako na jina la ukoo wako inayofanya kazi kwenye maisha yako sasa hivi—iwe unatambua au hutambui?


Kitabu kipya cha "Tambua Nguvu ya Asili Katika Maisha ya Mkristo" kinakuja kufua macho yako ya kiroho. Huu ni mwongozo wa kipekee unaokusaidia kuelewa jinsi asili yako ya kuzaliwa inavyofungamana moja kwa moja na maisha yako ya kila siku, ustawi wako, na safari yako ya kumwamini na kumtumikia Mungu.



Utakachokigundua na Kujifunza Ndani ya Kitabu Hiki:

  • Siri ya Ukoo na Kabila: Jinsi asili ilivyobeba damu yako na athari zake katika ulimwengu wa roho na mwili.
  • Nguvu ya Majina ya Urithi: Kuelewa jinsi jina ulilolibeba kupitia ukoo au ulilorithi kutoka kwa mtu mwingine linavyofunga au kufungua mambo yako.
  • Kuvunja Vifungo na Kuachilia Baraka: Jinsi ya kutambua asili zinazokuzuia na namna ya kuunganisha asili yako na nguvu ya Ukristo ili uishi maisha yenye ushindi.
  • Uhusiano wa Maisha na Imani: Kupata uelewa wa ndani kabisa wa jinsi ya kuishi maisha ya kawaida huku ukiwa na nguvu thabiti ya kiroho.


Mwandishi ELISHA CHUMA amekusanya hekima hii nzito na ya kiungu ili kukuweka huru. Ni matarajio yetu kuwa baada ya kusoma kurasa hizi, utafunguka kiakili na kiroho, na utajua namna bora ya kusimama kama Mkristo mshindi anayejitambua.


Usiendelee kuishi kwa kubahatisha. Fungua milango ya ufahamu wako leo na urudishe mamlaka ya maisha yako.

Frequently bought together

© 2026 Elisha Chuma. All Rights Reserved.

Powered By