SIRI YA MAFANIKIO YA BIASHARA DUKA LA REJAREJA TOLEO JIPYA 2025 & GENGE NDANI
Read Online

SIRI YA MAFANIKIO YA BIASHARA DUKA LA REJAREJA TOLEO JIPYA 2025 & GENGE NDANI

1
TSh10,000.00TSh15,000

PUNGUZO LA BEI KWA MUDA MFUPI ! (10,000/=)


Toleo jipya la kiteknolojia la kitabu hiki, “SIRI YA MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA NEW TECH EDITION 2026” Limekuja likiwa na ongezeko la Sura 2 mpya kabisa na kurasa 334 badala ya zile 184 za awali

 

Sura mpya ni “Mifumo mahsusi ya biashara ya duka la rejareja” na nyingine ni “Machimbo ya bidhaa za jumla Kariakoo na Mikoa yote Tanzania”. Kuna baadhi ya Sura za zamani pia zimeunganishwa kuwa moja

 

Maudhui ya zamani yote hayajabadilishwa bali kuboreshwa tu pale ilipohitajika mfano maelezo ya kina zaidi kwa mifumo ya madaftari (ya kianalojia)

 

Na kitu kikubwa sana kilichoongezwa ni hiyo mifumo hasa ya Kidijitali, Machimbo na Uzoefu wa mwandishi katika biashara ya Duka la rejareja ambao hapo awali haukuwekwa kikamilifu

 

Aidha unaweza kuona Tittle ya kitabu pale juu haijabadilika bado inasomeka “Toleo la mwaka 2025” na hii ni kwasababu hatujbadili link nzima ya kitabu kukwepa kutoonekana Google, ukibadili tittle na link (URL) hubadilika hivyo kuathiri SEO ya kitabu

 

Kitabu hiki hakikupi tu muongozo kamili, bali kinakufanya uwe Mtaalamu (Expert) kwenye biashara yako mwenyewe ya rejareja katika kudhibiti na kusimamia kikamilifu mapato yake msaidizi wako asikudokolee hata senti tano

 

Kimeainisha kwa njia rahisi mno mifumo yote ya usimamizi kuanzia ile ya kawaida ya madaftari mpaka ile ya kidijitali na akili mnemba / Artificial Intelligence (AI) 

 

Utafahamau kila dakika, kila saa na kila siku kabla hujaenda kulala umepata faida shilingi ngapi na siyo usubiri mpaka wiki au mwezi uishe

 

Hizi ni baadhi tu ya dondoo za yaliyokuwemo ndani ya kitabu:-

 

(1)     Mbinu za kutambua kama kila siku unapata faida au hasara bila kusubiri mwezi uishe au wiki

 

(2)     Mfumo rahisi wa kutambua na kuzuia udokozi wa msaidizi muda wowote

 

(3)     Njia nyepesi ya kudhibiti hesabu za duka unalouza wewe na msaidizi wako

 

(4)     Mifano ya madaftari ya kutunzia kumbukumbu na hesabu za duka lako

 

(5)     Nyenzo kuu 2 kila aliyetajirika kwa duka huzitumia

 

(6)     Kupiga stoku ya duka bila kupoteza muda mwingi

 

(7)     Maeneo hatari huwezi kufungua duka likakua

 

(8)     Mbinu za kupata mtaji na kiasi kizuri cha kuanzia

 

(9)     Makosa yanayoweza kuua duka lako hata kabla ya miezi 6 kuisha

 

(10)   Mbinu za kumfanya mteja arudi tena na tena

 

(11)   Vikwazo vikubwa 4 vinavyozuia watu kuanzisha maduka

 

(12)   Mbinu za kufufua duka lililozorota

 

(13)   Vitu vya kuangalia unapotaka kumuajiri mfanyakazi

 

(14)   Mchakato mzima wa kuajiri Mfanyakazi / Wafanyakazi ulivyo pamoja na Document / nyaraka mbili muhimu sana hupaswi kukosa kabisa kuzitumia katika mchakato huo na sample zake pia unazoweza kuziedit na kutumia moja kwa moja

 

(15)   Mbinu za kushindana na maduka makubwa yaliyokuzunguka hata kama la kwako ni dogo kiasi gani

 

(16)   Jinsi unavyoweza kuzitumia fursa zilizoletwa na akili bandia (AI) katika biashara yako ya rejareja

 

(17)   Njia bora za kukabiliana na wateja wakorofi

 

(18)   Jinsi ya kudili na chuma-ulete

 

(19)   Mpangilio wa duka unaovutia wateja na kukurahisishia kuuza

 

(20)   Kauli na vipeperushi vitakavyokufukuzia wateja na kudhani umelogwa

 

(21)   Mfumo wa mahesabu utakaokuwezesha kusimamia maduka zaidi ya 6 kwa wakati mmoja pasipo kuibiwa hata senti 5

 

(22)   Siri wenye maduka makubwa hawatakuambia kamwe hata uwape pesa.

 

(23)   Mchanganuo kamili wa biashara ya duka la rejareja na makisio ya hesabu za miaka 3

 

(24)   Jinsi ya kuanzisha na kuendesha biashara ya Genge kwa ufanisi

.

(25)   Aina za bidhaa za Genge zinazotoka haraka

 

(26)   Mifumo mikubwa 2 ya kudhibiti hesabu za Genge lako

 

(27)   Mfumo wa Dftari moja tu!

.

(28)   Siri kubwa 2 za kutunza matunda na mbogamboga zisiharibike upesi na kubakia na ubora wake wa asili pasipo kutumia wala friji

 

(29)   Mchanganuo kamili wa Biashara ya Genge

 

 

Kitabu hiki (E-book) unaweza kukipata hapa katika duka hili la mtandaoni mara tu unapolipia

 

Unaweza kulipia kupitia mtandao wako wowote wa simu ya mkononi unaotumia na kisha kupakua kitabu chako sasa hivi bila kusubiri.

 

Bofya neno BUY NOW kufanya malipo kwa Bei ya punguzo sh. 10,000/= muda mfupi bei ya kawaida sh. 15,000/= itarudi kama kawaida


Frequently bought together

© 2026 Peter Augustino Tarimo. All Rights Reserved.

Powered By